Home Habari za michezo BAADA YA KUTOKA SARE NA SIMBA…NABI ‘AVIMBA KWA HASIRA’…AWAPIGA BITI MASTAA YANGA…

BAADA YA KUTOKA SARE NA SIMBA…NABI ‘AVIMBA KWA HASIRA’…AWAPIGA BITI MASTAA YANGA…


Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amezuia mapumziko ya wachezaji wake mara baada ya mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba.

Hiyo ikiwa ni saa chache tangu timu hiyo itoke kuvaana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulichezwa juzi Jumamosi.

Kocha huyo amekuwa na utaratibu wa kutoa siku moja ya mapumziko kwa mastaa wake kila baada ya mchezo kumalizika kwa kuwaruhusu kurudi majumbani kwao kuangalia familia.

Lakini juzi Jumamosi imekuwa tofauti ni baada ya kocha huyo kuwataka wachezaji hao kurudi kambini Kijiji cha Avic Town na basi la timu kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Mrundi Cedric Kaze alisema kuwa kikosi hicho kimerejea kambini mara baada ya mchezo huo.

Kaze alisema kuwa wameumizwa na matokeo hayo ya suluhu waliyoyapata dhidi ya Simba kutokana na kutoyatarajia, wenyewe walihitaji pointi tatu pekee.

“Mechi ya 21 ya ligi tumetoka kucheza dhidi ya Simba, ilikuwa Kariakoo Dabi. Tulitamani kupata ushindi lakini hatukufanikiwa, siyo matokeo mazuri sana lakini hatukuyataka.

“Licha ya kuwepo kileleni tukimpita mpinzani wetu Simba ambaye yupo nafasi ya pili, hivyo hatutataka kuona tukitoka au kufungwa katika michezo ijayo.

“Michezo tisa imesalia, hakuna kupumzika tunarudi mazoezini leo (juzi Jumamosi) mara baada ya mchezo wa dabi kujiandaa na mchezo unaofuatia,” alisema Kaze.

SOMA NA HII  HUKI AKIWA KASIMAMISHWA ....'SURE BOY' HUYOOO ATUA YANGA KIMYA KIMYA..KUWA MBADALA WA AUCHO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here