Home Habari za michezo BAADA YA SAMATTA KUTUPIA MAGOLI 5 TU KWA MSIMU WOTE HUU…TIMU YAKE...

BAADA YA SAMATTA KUTUPIA MAGOLI 5 TU KWA MSIMU WOTE HUU…TIMU YAKE WACHUKUA UAMUZI HUU…


WAKATI ikiwa kwenye mchujo wa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji ‘Jupiler Pro, Royal Antwerp ambayo anaichezea nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ‘Samagoal’ imeripotiwa kuanza mzungumzo ya kumsajili kiungo fundi wa Toulouse ya Ufaransa, Branco van den Boomen.

Inaelezwa kuwa kocha wa chama la Samatta, Brian Priske amebaini kuwa na changamoto kwenye safu yake ya kiungo hivyo amewaagiza mabosi wa timu hiyo kumletea Mholanzi huyo ambaye ni chaguo lake la kwanza.

Licha ya van den Boomen kucheza Ligi Daraja la Kwanza Ufaransa ambalo ni maarufu kama Ligue 2, Priske anaamini kuwa fundi huyo anaweza kuwa suluhisho kwenye kikosi chake msimu ujao wa Jupiler Pro 2022/23.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa na msimu mzuri akiwa na Toulouse kwani ndani ya michezo 34 aliyocheza msimu huu, amepachika mabao 12 na kutoa asisti za mabao 21.

Van den Boomen amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho ambacho kinaongoza msimamo wa Ligue 2 kikiwa na pointi 76 kilizozikusanya kwenye michezo 35, na kinaongoza kwa utofauti wa pointi tano na Ajaccio yenye pointi 71 huku ikiwa mbele kwa mchezo mmoja.

Licha ya kuwa mbioni Toulouse kurejea Ligi Kuu Ufaransa, van den Boomen hana uhakika kuwa msimu ujao ataendelea kusalia kwenye klabu hiyo.

“Je, bado nitakuwa Toulouse mwaka ujao? Nafasi hiyo ni 50-50,” aliviambia vyombo vya habari vya Ufaransa.

Philippe Montanier, mchezaji wa zamani wa Standard na sasa kocha wa Toulouse, anatumai mchezaji huyo atasalia. “Itabidi tujaribu kusalia na wachezaji wetu bora, kwa sababu umoja wetu umetufanya kuwa na msimu wa kipekee. Tunajua kuwa ni ngumu ila tutajaribu.”

Ripoti zinasema kuwa ikiwa Antwerp inataka kumvutia zaidi Van den Boomen, inapaswa kuvunja benki kwa kuweka mezani kitita kikubwa cha fedha kama chambo cha kumnasa kirahisi kabla ya kunyekuliwa.

Toulouse inaweza kumruhusu Mholanzi huyo, ambaye ana mkataba hadi katikati ya 2023, aende kwa dau la kati ya euro 3-5 milioni. Hapo itafanya kupata faida kwa sababu Toulouse ilimchukua De Graafschap miaka miwili iliyopita kwa euro 350,000 tu.

SOMA NA HII  VITA YA UFUNGAJI HUKO LIGI YA MABINGWA AFRIKA SIO POA

Kama Royal Antwerp itamalizana na Van den Boomen itakuwa ni habari njema kwa Samatta na washambuliaji wengine wa chama hilo, ndani ya michezo 27 ya Jupiler Pro nahodha huyo wa Taifa Stars amepachika mabao matano tu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here