Home Habari za michezo BAADA YA SIMBA KUPATA SARE JANA…AHMED ALLY AIBUKA NA KULIA NA HILI…”YAMETUACHA...

BAADA YA SIMBA KUPATA SARE JANA…AHMED ALLY AIBUKA NA KULIA NA HILI…”YAMETUACHA NA HUZUNI..WANAMASONONEKO”…


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema hawajapendezwa na matokeo ya jana Jumatano (Mei 18) dhidi ya Azam FC, waliokua nyumbani kwao Azam Complex-Chamazi jijini Dar es salaam.

Simba SC ililazimisha sare ya 1-1, kufuatia bao la Nahodha na Mashambuliaji wao John Bocco alilofunga dakika chache baada ya Mshambuliaji Rodgers Kola kuifungia Azam FC kipindi cha kwanza.

Ahmed Ally amesema ilikua kama bahati mbaya kwao kushindwa kufikia lengo la ushindi, na ndio maana amekiri hawajapendezwa na kilichotokea Azam Complex usiku wa jana.

“Matokeo haya yamevuruga dhamira ya mipango yetu ya kupigania Ubingwa wetu msimu huu, ni matokeo ambayo kwa namna moja ama nyingine yamewaacha Wanasimba wakiwa na huzuni kubwa, yanawaacha Wanasimba wakiwa na butwaa kubwa, pia yanawaacha Wanasimba wakiwa na masononeko.”

“Malengo ya kupigania Ubingwa yanazidi kuwa magumu kwa Simba SC kwa sababu hizi sio nyakati za kupoteza mchezo, sio nyakati ya kupata sare, na sio nyakati ya kupata matokeo ya aina yoyote yake isipokua ushindi, na ndio maana mashabiki wa Simba SC wamekua na huzuni kubwa, wamekua wanyonge kwa sababu sio matokeo ambayo waliyatarajia kwa nyakati hizi.” Amesema Ahmed Ally

Kwa matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Azam FC, Simba SC imefikisha alama 50 zinazoendelea kuiweka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, huku Young Africans ikiwa kileleni kwa kumiliki alama 60.

Azam FC imefikisha alama 33 ambazo zinaiweka klabu hiyo ya Chamazi jijini Dar es salaam katika nafasi ya tano, ikitanguliwa na Geita Gold FC yenye alama 34 na Namungo FC yenye alama 36.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUPATA MDHAMINI MPYA....BOSI SportPesa AIBUKA NA HAYA....ADAI WALIFURAHI KUACHANA NAO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here