Home Habari za michezo BOCCO :- NILIPITA KIPINDI KIGUMU…MASHABIKI WANAPENDA KIZURI TU…UKIFANYA VIBAYA WANAKUKIMBIA…

BOCCO :- NILIPITA KIPINDI KIGUMU…MASHABIKI WANAPENDA KIZURI TU…UKIFANYA VIBAYA WANAKUKIMBIA…


Nahodha na Mshambuliaji wa Simba SC John Raphael Bocco amesema amedhamiria kumaliza msimu huu 2021/22 akiwa katika kiwango bora, baada ya kurejea kikosini.

Bocco alikuwa na wakati mgumu wa kucheza kwenye kikosi cha Simba SC msimu huu, kufuatia majeraha ya mara kwa mara kumuandama, hivyo ilimlazimu kukaa nje kwa muda mrefu kujiuguza.

Akizungumza baada ya kuifungia Simba SC bao la kusawazisha jana Jumatano (Mei 18) dhidi ya Azam FC, Mshambuliaji huyo amesema alipitia kipindi kigumu alipokua kwenye harakati za kujiuguza.

Amesema alitamani kuisaidia Simba SC lakini ilishindikana kwa hali iliyokua ikimkabili, lakini sasa amerejea hana budi kupambana na kufanikisha lengo la timu kisha lengo lake kama mchezaji.

“Nilipitia kipindi kigumu kidogo kutokana na majeraha. Mashabiki huwa wanapenda kitu kizuri. Ukifanya vyema watakusifu, ukifanya vibaya watakukimbia. Nataka kumaliza msimu na kiwango bora” amesema John Bocco

Hadi sasa Bocco ameshafunga mabao matatu tangu alipoanza kupewa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba SC, baada ya kupona majeraha, na anatarajia kuendelea kufanya hivyo katika michezo sita iliyosalia msimu huu.

SOMA NA HII  TFF WAANIKA SABABU ZA BARBARA KUZUIWA KUINGIA KWA MKAPA... ALITOA LUGHA CHAFU...