Home CAF MUSONDA:- NITAIBEBA YANGA MABEGANI…TP MAZEMBE NILIWAONYESHA…”MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA

MUSONDA:- NITAIBEBA YANGA MABEGANI…TP MAZEMBE NILIWAONYESHA…”MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA

MUSONDA NITAIBEBA YANGA MABEGANI...TP MAZEMBE NILIWAONYESHA...

Mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda ameapa kuhakikisha anafunga mabao muhimu yatakayoisaidia timu yake kufanya vizuri dhidi ya US Monastir.

Musonda ambaye ni ingizo jipya kwa Yanga mpaka sasa
amefanikiwa kuifungia timu hiyo bao moja katika Kombe la Shirikisho Afrika ambalo alifunga dhidi ya TP Mazembe.

Akizungumza nasi, Mshambuliaji huyo alisema kuwa: “Binafsi natamani kuona naisaidia Yanga kwa kufunga mabao muhimu katika mchezo wetu dhidi ya US Monastir, najua ni ngumu lakini nitajitahidi.

“Nilipofunga dhidi ya TP Mazembe nilijisikia vizuri, nilifahamu ulikuwa ni mchezo mgumu na muhimu kwetu Yanga, hivyo nilihisi kuwa niliwafurahisha sana Wanayanga.

“Hata katika mchezo wetu huu muhimu dhidi ya Monastir natamani kufunga ili niendelee kuwafurahisha Wanayanga na wazidi kuwa na imani na mimi, muhimu ni wao kuja kwa wingi uwanjani,” alisema mchezaji huyo.

SOMA NA HII  KIUNGO MGANDA AWACHANA MUDAHTIR NA BANGALA...AWATOBOLEA SIRI MECHI NA MAZAMBE