Home CAF BALEKE:- HOROYA WAULIZENI, MTIBWA SUGAR….”NITAHAKIKISHA NAPAMBANA…KWA MKAPA PATACHIMBIKA

BALEKE:- HOROYA WAULIZENI, MTIBWA SUGAR….”NITAHAKIKISHA NAPAMBANA…KWA MKAPA PATACHIMBIKA

Habari za Simba SC

Mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke amesema kuwa mara baada ya kufanikiwa kufunga mabao matatu ‘hat trick’ katika michezo ya ligi kuu, sasa ni zamu ya kufanya hivyo katika michezo ya kimataifa.

Baleke katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar wa ligi kuu alifanikiwa kuifungia Simba mabao matatu na kufanya kuwa hat trick yake ya kwanza tangia ajiunge na klabu hiyo Januari mwaka huu.

Akizungumza nasi, Baleke alisema kuwa: “Ni furaha kubwa sana kwangu kufanikiwa kufunga mabao matatu katika mchezo wangu uliopita, najua ni hat trick yangu ya kwanza lakini Wanasimba watarajie makubwa zaidi.

“Natamani kuona mabao haya matatu niyafunge katika michezo ya kimataifa kwa maana ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba tunashiriki, nitahakikisha napambana ili kufanya hivyo.

“Tunakwenda kucheza na Horoya, naamini tuna kikosi bora cha kupata matokeo dhidi ya Horoya, mimi kama mshambuliaji nikipata nafasi nitajitahidi kuisaidia timu ili kufanya vizuri na kupata ushindi katika mchezo wetu huu,” alisema mchezaji huyo.

SOMA NA HII  MASTAA WA YANGA HAWAAMBILIKI...MAYELE ACHACHAMAA...HUYO JOB SASA