Home Habari za michezo DABI YAMUACHA KANOUTE NA MAJANGA…’KAZI CHAFU’ YA AUCHO YAMUACHA NA KILIO KISICHOISHA…

DABI YAMUACHA KANOUTE NA MAJANGA…’KAZI CHAFU’ YA AUCHO YAMUACHA NA KILIO KISICHOISHA…


KIUNGO wa Simba, Sadio Kanoute alishindwa kuendelea na mechi ya dabi dhidi ya Yanga, baada ya kuchezewa rafu na kiungo, Khalid Aucho na kutolewa moja kwa moja nje ya uwanja.

Kanoute alisema baada ya tukio hilo aliumia sehemu ya chini ya mguu na kusikia maumivu makali yaliyomshinda kuendelea na mechi na hata siku ya Jumapili hakushinda vizuri nyumbani kwake.

Juzi (Jumatatu), alikwenda hospitali kufanya vipimo ili kufahamu shida pamoja na kuanza tiba haraka. “Baada ya vipimo nitafahamu shida niliyoipata pamoja na matibabu ambayo natakiwa kufanya ila tangu baada ya tukio nimekuwa nikisikia maumivu licha ya kufanya tiba zile za awali,” alisema Kanoute na kuongeza;

“Sijafahamu naweza kuwa nje kwa muda gani hadi nitakapopata majibu kutokana na vipimo vyangu.”

Kanoute alishindwa kusafiri na kikosi cha Simba  kilichokwenda Lindi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Ilulu.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MKUDE KUTEMWA SIMBA...MBRAZILI AKATA MZIZI WA FITINA...AANIKA MATATIZO YAKE...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here