Home Azam FC FT: AZAM FC 1-1 SIMBA SC….BOCCO KAWAOKOA TENA..MATUMAINI YA SIMBA YAZIDI KUYEYUKA…YANGA...

FT: AZAM FC 1-1 SIMBA SC….BOCCO KAWAOKOA TENA..MATUMAINI YA SIMBA YAZIDI KUYEYUKA…YANGA WANATAKA TISA TU…


MABINGWA Watetezi Simba wameshindwa kutamba ugenini dhidi ya Azam FC baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Chamazi Complex nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Azam FC walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Simba katika dakika ya 17 bao likifungwa na Mshambuliajia Rodgers Kola,Mshambuliaji wa zamani wa Azam ,John Bocco aliisawazishia timu yake dakika ya 44.

Kipindi cha pili timu zote ziliafanya mabadiliko na kuanza kushambualiana kwa zamu hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zimeweze kugawa pointi moja moja.

Kwa Matokeo hayo Simba wamefikisha Pointi 50 wakizidiwa Pointi 10 na Vinara wa Ligi hiyo Yanga wenye Pointi 60 ,Timu zote zikiwa zimecheza mechi 24 na kubakiwa na mechi sita huku Azam FC wakibaki nafasi ya tano wakiwa na Pointi 33.

Ndio kusema kwamba, Yanga wanahitaji alama tisa tu sawa na ushindi wa mechi tatu zijazo ili waweze kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu .

SOMA NA HII  RAIS SAMIA 'ATIA MKONO' UWANJA WA YANGA JANGWANI....BENKI YA DUNIA KUMWAGA MABILIONI...