Home Habari za michezo GEITA GOLD YAWASHA TAA MCHANA….WAIKUNG’UTA KAGERA ‘CHA UCHUNGU’…MPOLE NA MAYELE SAWA TU…

GEITA GOLD YAWASHA TAA MCHANA….WAIKUNG’UTA KAGERA ‘CHA UCHUNGU’…MPOLE NA MAYELE SAWA TU…


Klabu ya soka ya Geita Gold imefanikiwa kuingia nne bora kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara kufuatia matokeo ya ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera.

Geita Gold inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania bara kwa mara ya kwanza kwenye historia yao walipata bao hilo pekee na la ushindi lililofungwa na George Mpole ambaye amefikisha bao la 12 na kuwa kinara wa kufumania nyavu sawa na nyota wa Yanga ,Fiston Mayele.

Chini ya Kocha, Fredy Felix Minziro, Geita Gold imejipambanua kwa kufanya vyema katika mechi zake huku ikionyesha upinzani mkubwa dhidi ya vigogo Simba na Yanga katika mechi zake.

Mwanzoni mwa msimu timu hiyo iliyokuwa inanolewa na Kocha, Etiene Ndayiragije ilikuwa na mwenendo mbaya kiasi cha kuhatarisha uwepo wao kwenye Ligi msimu ujao, ndipo Uongozi wa wachimba madini hao walipoamua kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi pamoja na usajili wa wachezaji wenye uzoefu na Ligi akiwemo beki Kelvin Yondana na Juma Nyoso.

Kwa mwenendo huu upo uwezekano wa Geita Gold kumaliza ndani ya timu nne bora na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa kama ilivyokuwa kwa Biashara Mara United.

SOMA NA HII  KISA MATOKEO MABAYA..VIGOGO SIMBA WASHINDWA KUJIZUIA...WAWAVAMIA WACHEZAJI NA KUWAPIGA 'BITI LA KUFA MTU'..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here