Home Habari za michezo KIPIGO KUTOKA REAL MADRID CHAMVURUGA GUARDIOLA…AGOMA KUZUNGUMZA NA WACHEZAJI WAKE….

KIPIGO KUTOKA REAL MADRID CHAMVURUGA GUARDIOLA…AGOMA KUZUNGUMZA NA WACHEZAJI WAKE….


Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi kuwa mpaka sasa bado hajazungumza na wachezaji wake kuhusu lililotokea kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa.

kikosi cha Pep Guardiola walisafiri hadi Hispania huku wakiwa na faida ya kushinda mchezo wa kwanza kwenye uwanja wao wa nyumbani, na mchezo walianza vizuri kwa kupata goli la kuongoza kutoka kwa Mahrez, baadae Rodrygo aliharibu kwa kufunga mara mbili kabla ya karimu Benzema kufunga kwa mkwaju wa penati kwenye dakika za nyongeza.

Kesho ni siku ya kwanza ambayo tunakutana kama timu, kwa pamoja na kuzungumza kama timu, nini tumefanya kwenye nusu fainali, ni wapi tuko vizuri sio tu kwenye hii michezo miwili lakini kwa msimu mzima.

“Huenda ndicho kipindi ambacho najivunia sana tangu kuwa kocha kuwa kwenye klabu hii na taasisis, na hadi siku ya mwisho kuwa hapa, tunajitoa kwa pamoja.” alisema Pep Guardiola

“Baada ya mchezo huu tunafahamu kuwa kuna michezo minne ya ligi kuu imebako, akili yaetu imejikita sehemu nyepesi ni dhidi ya Newcastle, hakuna zaidi ya hapo.” aliongezea Pep Guardiola

SOMA NA HII  AHMED ALLY: AL AHLY, MAMELOD, ZAMALEKH NA MAZEMBE WANASUBIRI KWA HAMU KUJUA USAJILI WETU MSIMU HUU...