Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA YANGA J/MOSI….BARBARA ‘AMPIGA MKWARA’ PABLO…AMWAMBIA USHINDI LAZIMA…LA SIVYO…

KUELEKEA MECHI NA YANGA J/MOSI….BARBARA ‘AMPIGA MKWARA’ PABLO…AMWAMBIA USHINDI LAZIMA…LA SIVYO…


Simba imefafanua hali za Shomari Kapombe, Aishi Manula na Clatous Chama kuelekea mechi ya Jumamosi kwenye nusu fainali ya FA itakayopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Lakini Mwanaspoti linajua Kocha Pablo Franco ameambiwa hivi, “hakuna namna lazima ushinde hii mechi.”

Meneja wa mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa: Manula aliyeumia vidole viwili vya mkono wa kulia alisema; “Amefanya mazoezi lakini si ya kudaka mipira bali kuchezea tu mpira kwa miguu, leo (jana) ataanza ya kudaka maana kidonda chake kinaendelea vizuri.”

“Shomary Kapombe ambaye anasumbuliwa na nyama za paja siku mbili hizi (juzi na jana) hajafanya mazoezi labda kesho (leo) anaweza kuanza hivyo tunategemea pia kwenye mechi huenda akacheza maana majeruhi yake haikuwa kubwa sana,” alisema na kuongeza kuwa Erasto Nyoni naye yuko fiti na anakiwasha kwelikweli.

“Clatous Chama jana (juzi) alianza mazoezi ya peke yake ila huyu itategemea na maendeleo yake zaidi hadi siku hiyo lakini kwa ufupi anaendelea vizuri tofauti na mwanzo, alipewa mwezi mmoja kuwa nje lakini ikiwa na maana ya pamoja na siku za matazamio ya afya yake.”

LAZIMA MSHINDE

Habari za uhakika zinadai kwamba uongozi wa Simba umekaa kikao kizito na Benchi la Ufundi wakilitaka lifanye kila jitihada kuhakikisha wanaifunga Yanga na kutinga fainali za michuano hiyo Jumamosi.

Habari zinasema, Juzi Jumatatu, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisafiri hadi jijini humo kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye mambo ya utawala lakini kitu cha kwanza kukifanya ni kukutana na benchi la ufundi chini ya kocha Pablo Franco.

Imeelezwa kuwa matokeo wanayopata kwenye ligi ni wazi yamewakatisha tamaa ya kutetea ubingwa wao kutokana na watani wao kuwa juu kwa pointi 63 huku wao wakiwa na pointi 51, wote wamebakiwa na mechi tano.

Habari zaidi zinadai kuwa kikao hicho kilichochukuwa muda mrefu wa zaidi ya saa mbili, msisitizo ukiwa ni mechi hiyo ambayo wanaitolea macho kwani wakikwama basi msimu huu hawatukuwa na kombe kubwa Bara ukiachana na kombe lao la Mapinduzi.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA...MTIBWA WAHAMISHIA MECHI UWANJA AMBAO SIMBA WALIFUNGWA GOLI 3..

Alipoulizwa, Ahmed Ally kuhusiana na hilo alikiri kuwepo kwa kikao hicho. “Ni kweli CEO alikutana na Benchi la Ufundi na kuzungumza nao mambo mbalimbali hasa kuelekea mchezo huo wa Jumamosi, FA ndiko hasa ambako matumaini yetu yalipo kwasasa hivi ni kutaka kuhakikisha wanashinda.

“Amewaambia kuwa ushindi upatikane, hivyo wao kama wataalamu wa benchi la ufundi wana kila sababu ya kupambana kuhakikisha ushindi unapatikana, maana huo ndiyo ubingwa pekee tunaotakiwa kuutetea msimu huu na si vinginevyo,” alisema Ahmed.

Simba tayari ina uhakika wa kushiriki michuano ya kimataifa inayoanza mapema mwezi Septemba mwaka huu na tayari wameanza kufanya usajili wa maana.