Home Habari za michezo PAMOJA NA KUSEMA KUWA AMEPONA…YANGA WAANIKA MUSTAKABALI WA YACOUBA…DAKTARI AFICHUA YA NYUMA...

PAMOJA NA KUSEMA KUWA AMEPONA…YANGA WAANIKA MUSTAKABALI WA YACOUBA…DAKTARI AFICHUA YA NYUMA YA PAZIA…


Yanga iko Kanda ya ziwa kwa maandalizi ya kuelekea mchezo dhidi ya Simba wa Nusu Fainali ya Kombe la Azam Shirikisho (ASFC) wakiwa na mshambuliaji wao Yacouba Sogne ambaye hajacheza msimu huu kutokana na majeruhi sasa imefahamika atarudi uwanjani lini.

Akizungumza daktari wa Yanga, Youssef Mohamed alisema mshambuliaji huyo anaweza kuwa sehemu ya kikosi hicho katika mechi mbili za mwisho za ligi dhidi ya Mbeya City na Mtibwa Sugar.

β€œUnaona tunasafiri naye sasa ni kutokana na tunataka aanze kujiona yuko sawa na wenzake na taratibu atacheza mpira na wenzake,” alisema Youssef na kuongeza;

β€œKabla ya ligi kufungwa atacheza au atakuwa sehemu ya kikosi katika mechi mbili za mwisho tunafurahi kuona maendeleo yake yamekuwa mazuri sana na alizingatia kila hatua ya matibabu yake.

Yanga bado inapiga hesabu za jinsi ya kubaki na straika huyo raia wa Burkina Faso ingawa uhakika watamuongezea mkataba baada ya awa wali kuisha mwisho wa msimu.

SOMA NA HII  NEEMA ZAZIDI KUMIMINIKA YANGA....WASAINI MKATABA WA KUIPA KLABU MABILIONI YA PESA KAMA SIMBA....KAZI NDIO INAANZA...