Home Ligi Kuu BUSWITA: HATUKUWA NA CHA KUPOTEZA NDANI YA UWANJA

BUSWITA: HATUKUWA NA CHA KUPOTEZA NDANI YA UWANJA


 PIUS Buswita, nyota wa kikosi cha Polisi Tanzania amesema kuwa kwenye mchezo wao wa jana Machi 7 hawakuwa na cha kupoteza jambo lililowafanya wapambane mwanzo mwisho kupata matokeo chanya.

Wakati ubao dakika 45 za mwanzo ukisoma Polisi Tanzania 0-1 Yanga, bado vijana wa Malale Hamsini waliongeza juhudi kipindi cha pili kusaka ushindi wakiwa nyumbani.

Ulikuwa ni mchezo wao wa mzunguko wa pili baada ya ule wa kwanza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru.

Ni Yanga walianza kupachika bao la kwanza dakika ya 41 kupitia kwa Fiston Abdulazack kisha Buswita aliweka mzani sawa dakika ya 89 na kufanya timu zote kugawana pointi mojamoja.

Matokeo hayo ya sare ya kufungana baoa 1-1 yalikwenda na kibarua cha benchi zima la ufundi la Yanga ambalo linaongozwa na Cedric Kaze.

 Buswita amesema:”Hatukuwa na cha kupoteza baada ya kufungwa bao la mapema kipindi cha kwanza jambo ambalo lilitufanya tuongeze nguvu kwenye kusaka ushindi.

“Baada ya kupambana mwisho wa siku tukapata hicho ambacho tupo nacho mkononi hivyo kwetu hakuna ubaya tunazidi kupambana kusaka ushindi ndani ya uwanja,” amesema.

SOMA NA HII  KOCHA MTIBWA SUGAR AMLILIA BEKI WAKE WA YANGA