Home Uncategorized MABINGWA SIMBA WAANZA NA MKWARA HUU

MABINGWA SIMBA WAANZA NA MKWARA HUU

BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba kurejea kutoka Afrika Kusini, Kocha Mkuu Patrick Aussems amesema kuwa kazi ndo kwanza inaanza.

Simba ilikweka kambi nchini Afrika Kusini ambayo imetumia muda wa wiki mbili kwa sasa wamerejea Bongo kwa maandalizi ya msimu ujao.

“Tumemaliza salama kazi yetu ya kwanza ambayo ilikuwa ni maandalizi na sasa kikubwa tunaendelea vizuri hivyo kazi yetu kubwa ni kuendelea kile ambacho tumejifunza,

“Kwanza ratiba yetu inatutaka uanze kwenye Ligi ya Mabingwa jao ni muda mfupi nina imani tutafaya vizuri, kikubwa ni kwamba kila mmoja amefurahi nasi tutapambana,” amesema.

 Agosti sita, Simba itacheza mchezo wa kirafiki na Power Dynamo ambao ni maalumu kwa ajili ya kutambulisha wachezaji na uzi mpya wa Simba na ni wiki maalumu iliyopewa jina la SportPesa Simba wiki.

SOMA NA HII  HIZI HAPA DAKIKA 90 ZA MAAMUZI MAGUMU NA YANGA