Home CAF MWAMUZI WA SIMBA DHIDI YA KAIZER HUYU HAPA

MWAMUZI WA SIMBA DHIDI YA KAIZER HUYU HAPA


PACIFIQUE Ndabihawenimana mwenye umri wa miaka 36, ndiye anatajwa kusimama kuamua vita ya kesho kati ya Simba dhidi ya Kaizer Chiefs katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mburundi huyo anatajwa kuwa na rekodi ya msimamo mkali na urahisi wa kutoa adhabu ikiwemo kadi za njano na nyekundu, lakini pia kuhimili presha ya mchezo.

Simba Jumamosi iliyopita wakicheza ugenini katika uwanja wa FNB (Soccer City), katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika walikumbana na kipigo cha mabao 4-0 ambayo yameweka rehani nafasi yao ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

Simba ina deni kubwa la kuhakikisha wanashinda mchezo wa kesho Jumamosi kwa tofauti ya mabao 5-0 ili kufufua matumaini yao ya kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

SOMA NA HII  'AS VITA TUPO TAYARI KUFUNGWA KESHO'