Home news ILE ISHU YA NTIBAZONKIZA KUTAKIWA NA TIMU YA UARABUNI IKO HIVI…YANGA WATOA...

ILE ISHU YA NTIBAZONKIZA KUTAKIWA NA TIMU YA UARABUNI IKO HIVI…YANGA WATOA TAMKO….


TAARIFA zinasema kwamba, Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ wamemfuata nyumbani kwao Burundi na viongozi wa timu moja kutoka Uarabuni kwa ajili ya mazungumzo ili kumsajili. 

Saido ambaye hivi karibuni aliondoka Tanzania kwenda Burundi kwa ajili ya mapumziko mafupi, wakati akiwa huko ndipo Waarabu hao walipomuibukia kwa nia ya kumshawishi wamsajili.

Nyota huyo aliyetua Yanga dirisha dogo la msimu uliopita, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Mtu wa karibu na mchezaji huyo, amesema kwamba: “Hivi karibuni Saido akiwa kwao Burundi alifanya kikao na mwakilishi wa timu kutoka Uarabuni ambayo siwezi kuitaja.

“Anaweza kukubali dili hilo maana lina pesa nyingi, ila kwa upande wa viongozi wa Yanga wamemwambia asubiri wakimaliza Mapinduzi wataongea naye kujadili mkataba mpya.”

Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema: “Kuhusu suala la Saido lazima ataongezewa mkataba.”

SOMA NA HII  MAYELE, CHAMA NA LUSAJO WAGOMBANISHWA...MMOJA KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI HUU...