Home Uncategorized RUVU SHOOTING YAWABANA WAJEDA MABATINI, WAACHA POINTI TATU

RUVU SHOOTING YAWABANA WAJEDA MABATINI, WAACHA POINTI TATU


 
OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameweka wazi kwamba malengo yao makubwa kwa msimu huu wa 2020/21 ni kuweza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.


Leo Novemba 25 imeibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa ligi, mbele ya Tanzania Prisons.

Nyota wa Ruvu Shooting, Abrahman Mussa amepachika bao la ushindi leo mbele ya Tanzania Prisons,  Uwanja wa Mabatini.


Bao pekee la ushindi limepatikana dakika ya 30 na kuifanya timu ya Ruvu Shooting kusepa na pointi tatu mazima.


Mussa anafunga kwenye mechi mbili mfululizo ambazo ameanza kucheza kwenye kikosi chake bao lake la kwanza ilikuwa mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Uhuru,Novemba 20.

Ushindi huo unaifanya Ruvu kufikisha jumla ya pointi 22 ikiwa nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 12.


SOMA NA HII  BENCHIKHA AFUNGUKA JINSI WATAKAVYOCHUKUA POINTI TATU MBELE YA WYDAD