Home Uncategorized LUIS MIQUSSONE KINARA WA PASI ZA MWISHO BONGO AJIPA KAZI NGUMU

LUIS MIQUSSONE KINARA WA PASI ZA MWISHO BONGO AJIPA KAZI NGUMU


LUIS Miquissone ambaye ni kinara wa pasi za mwisho ndani ya Klabu ya Simba inayoongozwa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck amejipa kazi ngumu ya kufanya kwa ajili ya kufikia malengo aliyojiwekea pamoja na timu kiujumla. 


Ikiwa imefunga mabao 29 amehusika kwenye mabao saba akifunga bao moja na kutoa pasi sita za mabao.


Bao lake la kwanza aliwafunga JKT Tanzania Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na alionyeshwa kadi yya njano kutokana na kushangilia kwa nguvu na kuwafuata mashabiki wake.


Luis ambaye ni raia wa Msumbiji amesema kuwa ana kazi ngumu ya kufanya ndani ya kikosi hicho ambacho kinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni pamoja na kutengeneza nafasi za kufunga pamoja na kufunga mabao.


“Kazi ni kubwa na mwanzo mzuri siku huwa unafurahisha, licha ya kufunga na kutengeneza nafasi za mabao bado kuna kazi ya kuendelea kufanya ili kuwa bora zaidi.


“Tunatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu inashinda na kupata matokeo ili hayo yatokee lazima kila mmoja atimize majukumu yake ndani ya uwanja. Hivyo kikubwa tutaendelea kupambana na tunahitaji sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  LIVERPOOL V ARSENAL NI BALAA KESHO, REKODI ZAIBEBA TIMU HII HAPA