Home Uncategorized BERNARD MORRISON WA SIMBA APOTEZWA NA MZAWA JUMLAJUMLA

BERNARD MORRISON WA SIMBA APOTEZWA NA MZAWA JUMLAJUMLA


 BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Simba ambaye alisajiliwa kwa dili la miaka miwili akitokea Klabu ya Yanga amepata mbabe wake ambaye amejibu mapigo yake na kumpoteza kwa rekodi.

Simba ilivutiwa na uwezo wa Morrison ambaye alianza kuonyesha akiwa Yanga ikiwa ni pamoja na kupanda mpira alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Mkapa kwenye Kombe la Shirikisho wakati Yanga ikishinda mabao 2-0.

Kwenye mchezo huo Morrison alifunga bao moja na timu yake. Akiwa ndani ya Simba, Morrison ameendeleza makeke yake ya kupanda juu ya mpira ambapo alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa ilishinda mabao 4-0.

Katika mchezo huo Morrison aliishia kupanda mpira na hakuweza kutoa pasi ya bao wala kufunga bao. Pia alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati Simba ikishinda mabao 7-0, alipanda mpira na alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

Rekodi yake kwa msimu wa 2020/21 imejibiwa kibabe na mzawa Abrahaman Mussa ambaye alikuwa nyota wa mchezo wakati timu yake ya Ruvu Shooting ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City.

Mussa alifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao akimpa moja Fully Zully Maganga na William Patrick na kuipoteza rekodi ya Morrison ambaye akiwa Simba aliishia kutembea juu ya mpira huku akitoa pasi moja ya bao na kufunga bao moja.

Jumla, Mussa amefunga bao moja na kutoa pasi tatu za mabao huku timu yake ikiwa imefunga mabao 11 na pointi 19, Morrison ametoa pasi mbili za mabao kati ya mabao 29 yaliyofungwa kwa msimu wa 2020/21 huku yeye akifunga bao moja.


Kwenye mabao 29 Morrison amehusika kwenye mabao matatu huku mzawa Mussa akihusika kwenye mabao manne kati ya 11.

 

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA KMC