Home Uncategorized YANGA YATOA TAMKO KUHUSU ISHU YA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

YANGA YATOA TAMKO KUHUSU ISHU YA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze amesema ikiwa wataendelea kupata matokeo mazuri katika kila mchezo wa Ligi Kuu Bara msimu huu basi hakuna atakayeweza kuzuia ubingwa ndani ya kikosi hicho kutokana na ubora waliokuwa nao.

 

Yanga chini ya Kaze imeweka rekodi ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ikiwa nafasi ya kwanza na kutopoteza mchezo hata mmoja.


Imecheza jumla ya mechi 18 imekishinda mechi 13, imekusanya sare mechi tano huku na ina pointi 44.

 

 Kaze amesema ana matumaini makubwa ya kuweza kuchukua ubingwa wa msimu huu ikiwa wachezaji wake wataendelea kujituma kwa kupata matokeo mazuri katika mechi za mzunguko wa pili baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza.

 

“Kitu kikubwa kwetu ni jinsi gani tunaweza kuendelea hapa tulipoishia katika mzunguko wa kwanza, najua ligi imekuwa ngumu na ushindani unaongezeka kadiri unavyokutana na timu nyingine ambayo nayo imekuwa ikihitaji kupata matokeo mazuri dhidi yetu.

 

“Tunataka ubingwa wa msimu huu kwa kuwa ni jambo ambalo linawezekana ingawa mzunguko wa pili unakuwa mgumu zaidi lakini hatuwezi kuacha malengo yetu ya ubingwa kwa kuwa ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu,” amesema Kaze.


Safu ya ushambuliaji ya Yanga imefunga mabao 29 na kwenye mabao hayo aliyehusika kwenye mabao mengi ni Yacouba Sogne ambaye amefunga mabao manne na kuto pasi nne za mabao.


Ditram Nchimbi mwili jumba mzawa huyu ametoa pasi moja ya bao alimpa Michael Sarpong ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.

SOMA NA HII  SABABU YA AZAM FC KUKOSA UBINGWA WA KAGAME HII HAPA