Home Habari za michezo NI BOCCO TENA….REKODI YAKE YAZIDI KUWA NGUMU BONGO…MASTAA LIGI KUU WAJITOKEZA KUMSEMEA….

NI BOCCO TENA….REKODI YAKE YAZIDI KUWA NGUMU BONGO…MASTAA LIGI KUU WAJITOKEZA KUMSEMEA….

TULIWAAMBIA! Kauli za baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu Bara, wakimzungumzia Nahodha wa Simba, John Bocco dhidi ya kejeli za mashabiki waliokuwa wakimbeza kabla ya kuanza kucheka na nyavu.

Bocco alifunga mabao matatu (kabla ya mechi ya jana dhidi ya Geita Gold) kwenye Ligi Kuu Bara, jambo lililomuibua straika wa Kagera Sugar, Hamisi Kiiza akisema hakuwahi kuamini kama staa huyo wa Simba ameishiwa kiwango ghafla.

“Muda ni hakimu wa haki, niliwaambia tangu mwanzo kwamba Bocco bado ni fundi wa kucheka na nyavu na ana heshima kubwa Tanzania, maana ndiye anayeongoza kwa mabao mengi kwa wachezaji wanaocheza sasa, mchezaji kama huyo huwezi kumuona ameisha kirahisi,” alisema.

Alisema Bocco anastahili heshima yake, kutokana na rekodi ya kipekee ya mabao mengi aliyonayo (145) tangu aanze kucheza Ligi msimu wa 2008 hadi 2022.

“Haiwezekani msimu ulioisha Bocco alimaliza na mabao 16 ghafla tu aonekane hana lolote, ila ninachojua mashabiki wakikuchoka hata ufanye kitu gani inakuwa ngumu kukuvumilia nyakati ngumu,” alisema.

Hoja ya Kiiza iliungwa mkono na kipa wa KMC, Farouk Shikalo ambaye kabla ya Bocco kuanza kufunga, alimkingia kifua akisema bado ni straika hatari, hivyo aliwakumbusha waliombeza kuanza kuhesabu mabao yake kwa sasa.

“Bocco bado ni straika makini na anayelijua goli, lilikuwa suala la muda kuanza kucheka na nyavu, kabla msimu haujaisha ameanza kufunga, hilo linatufunza kwamba kuna wakati mchezaji anakuwa na upepo mbaya,” alisema.

Yalivyopatikana mabao 145 ya Bocco na kwenye mabano ni idadi ya mabao kila msimu, akiwa Azam FC msimu wa 2008/09 (1), 2009/10 (14), 2010/11 (15), 2011/12 (19), 2012/13 (7), 2013/14 (7), 2014/15 (3), 2015/16 (12), 2016/17 (10), akiwa na timu hiyo yalikuwa jumla ya mabao 88.

Alipohamia Simba msimu wa 2017/18 (14 ), 2018/19 (15), 2019/20 (9), 2020/21 (16) na 2021/22 hadi sasa ana (3), hivyo Simba kabla haujamalizika msimu huu ana jumla ya mabao 57.

SOMA NA HII  UBABE WA YANGA WAIHAMISHA GEITA GOLD