Home news MBEYA KWANZA KUANZA MAZOEZI KESHO

MBEYA KWANZA KUANZA MAZOEZI KESHO


KESHO Oktoba 7 kikosi cha Mbeya Kwanza kinatarajiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo imeanza vizuri mechi za awali ambapo mchezo wake wa kwanza ilishinda mbele ya Mtibwa Sugar bao 1-0 na ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Mbeya Kwanza.

Katika mchezo wa Dabi ya Mbeya ushindani ulikuwa mkubwa na Mbeya Kwanza walipindua meza kibabe na kufanya ubao kusoma Mbeya City 2-2 Mbeya Kwanza.

Mabao yote ya Mbeya Kwanza yalifungwa na Crispian Ngushi ambaye alifunga bao bora kwa mzunguko wa pili kwa mtindo wa Acrobatic.

Taarifa rasmi kutoka Mbeya Kwanza imeeleza kuwa kesho kikosi kinatarajiwa kuanza mazoezi baada ya wachezaji kupewa mapumziko ya muda wa siku tatu.


 

SOMA NA HII  KIFAA CHA MAZEMBE CHAKUTANA NA 'NKONO WA NTU' YANGA....AUMWA GHAFLA...ACHUJWA RASMI...