Home Habari za michezo MWAMBUSI AINGILIA USAJILI YANGA…AWACHANA GSM KUHUSU KUSAJILI MASTAA WA MAANA…”WAVUNJE BENKI”…

MWAMBUSI AINGILIA USAJILI YANGA…AWACHANA GSM KUHUSU KUSAJILI MASTAA WA MAANA…”WAVUNJE BENKI”…


KLABU ya Yanga msimu ujao wa michuano ya kimataifa inatarajiwa kuiwakilisha nchi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kocha wa zamani wa timu hiyo, Juma Mwambusi amewauma sikio kwa kuwapa mchongo wa maana ili kuweka heshima.

Mwambusi aliyewahi kuwa kocha msaidizi na baadaye mkuu wa muda wa Yanga, mbali na kuzinoa Mbeya City aliyoipandisha Ligi Kuu misimu sita iliyopita, alisema ili Yanga ifanye vyema kimataifa ni lazima iongeze majembe ya maana.

kocha huyo aliyewahi kuzinoa pia Moro United na Azam alisema licha ya Yanga kufanya vizuri msimu huu, lakini inahitaji kuongeza wachezaji katika baadhi ya nafasi ili kuimarisha kikosi kitakachoibeba ya kimataifa.

“Langoni wala hakuna haja ya kuongeza mtu, kwani waliopo wapo vizuri, ila kwenye ulinzi kwa sababu tunaenda michuano ya kimataifa Yanga inahitaji kuongeza wachezaji katika maeneo mengi hata katikati wakiongeza mtu mmoja na kule mbele wapatikane straika na winga mpya mkali zaidi ya waliopo sasa,” alisema.

“Tunataka mtu aliyekamilika kwa sababu mtu anayepata nafasi kikosi cha kwanza, lazima awe mwenye uwezo na atakayeifaa timu. Kiwango ni lazima kiwepo kwa wachezaji watakaosajiliwa sijui kama kuna viongozi walienda katika ile Afcon kwani kuna wachezaji wanacheza ligi za ndani kama Mali wapo vizuri, lakini ndio wachezaji bora ambao wanaweza kucheza katika ligi yetu.”

Mwambusi alisema kama timu inaenda kucheza na klabu za kiwango cha Al Ahly na Mamelodi Sundowns inatakiwa kwua na wachezaji wazuri na ni lazima kuvunja benki ili kuwanasa. Msimu huu Yanga iling’olewa raundi ya kwanza kwa kufungwa mabao 2-0 na Rivers United ya Nigeria, ikilala bao 1-0 nyumbani na ugenini.

Akiizungumzia Ligi Kuu, Mwamusi alisema: “Imekuwa na ushindani, nami kinachonifurahisha kila timu inacheza inataka matokeo ni jambo kubwa.”

SOMA NA HII  WAKATI NABI AKITAJWA KUPEWA ULAJI TAIFA STARS...TFF WAIBUKA NA KUANIKA UKWELI ULIVYO...