Burudani

BAADA YA KUMALIZANA NA KAJALA…HARMONIZE AIBUKA NA UJUMBE HUU KWA SAMATTA…AMSHUSHIA DONGO ALLY KIBA..

admin June 14, 2022 7:52 am


Harmonize au Teacher Konde; ni staa wa muziki kutoka kiwanda cha Bongo Fleva ambaye ameonesha nia yake ya kushiriki katika mchezo wa Tamasha la Samakiba ambalo ni ‘projekti’ inayoendeshwa na Mfalme wa Bongo Fleva, King Kiba na staa wa soka wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta.

Lengo la Samakiba ambalo hufanyika kila mwaka baada ya kumalizika kwa msimu wa soka ni kuchangia elimu nchini Tanzania.

Harmonize anasema; “Samatta msanii wako namkabia juu kabisa havuki nusu uwanja, halafu nakuwekea mtambaliko kama Sure Boy, nataka uniwekee wanangu, Jonas Mkude, Feisal pale dimbani, kushoto niwekee Chilunda, kulia niwekee Idd Nado.”

Ujumbe huo unamaanisha kwamba Harmonize ameomba nafasi kwenye timu Samatta ambapo atakuwa mpinzani wa King Kiba wakiwa uwanjani.

Kumbuka King Kiba ndiye msanii pekee wa Bongo Fleva aliyewahi kushiriki Ligi Kuu ya Tanznaia Bara akikipiga katika Klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga.

Swali wanalojiuliza wengi ni kwamba, je, Harmonize ataweza kumkaba King Kiba huku wote wakiwa wanaendelea na mazoezi ya gym?

KUHUSU KUKIPIGA MSIMBAZI MSIMU UJAO…SAIDO NTIBAZONKIZA AFUNGUKA A-Z WALICHOAFIKIANA NA MABOSI… ISHU YA MOSES PHIRI NA SIMBA…? UKWELI WOTE HUU HAPA…HAKUNA JIPYA NI YALE YALE..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply