Habar za Usajili Simba

ISHU YA MOSES PHIRI NA SIMBA…? UKWELI WOTE HUU HAPA…HAKUNA JIPYA NI YALE YALE..

admin June 14, 2022 11:26 am

 


Taarifa za uhakika kutoka ndani ya klabu ya Simba zinaeleza kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Moses Phiri (27) amejiunga na miamba hiyo ya Msimbazi.

Nyota huyo wa Klabu ya Zanaco ya Zambia amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Simba SC na anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Phiri ambaye alikuwa mfungaji Bora wa ligi kuu ya Zambia msimu wa 2020/2021 akiwa na magoli 13.

Inaelezwa kuwa, Phiri anakwenda kuchukua nafasi ya Mkongomani, Chris Mushimba Mugalu (31) ambaye anadaiwa Simba itaachana naye kutokana kiwango chake kutoridhisha msimu huu unaomaliza.

Habari za Phiri kusajiliwa na Simba si geni, kwani ilifaamika kitambo kuwa nyota huyo angetua msimbazi kutokana na kuwa alishasaini mkataba wa awali, kitu ambacho kiliinyong’onyeza Yanga na kuamua kuachana naye.

Mchezaji huyo atakumbukwa na wengi mara baada ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa kirafiki na Yanga, kwenye kilele cha siku ya wananchi mwanzoni mwa msimu huu.

Wachezaji wanaowindwa na Simba mpaka sasa 1. Ceasar Manzoki – Straika 2. George Mpole – Straika 3. Morlaye Sylla – Kiungo 

DONE DEAL 

1. Moses Phiri – Straika.

BAADA YA KUMALIZANA NA KAJALA…HARMONIZE AIBUKA NA UJUMBE HUU KWA SAMATTA…AMSHUSHIA DONGO ALLY KIBA.. BAADA YA KUMALIZANA NA AZIZ KI….TARAJIA KUONA ‘VITASA HIVI VYA KAZI CHAFU’ KUTUA YANGA MSIMU UJAO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply