Habari za michezo

BAADA YA KUONDOKA SIMBA NA KUJIUNGA NA AMAZULU….BWALYA AFUNGUKA A-Z KUHUSU USAJILI HUO…

admin June 27, 2022 9:00 am


Kiungo aliyedumu akiwa na uzi wa Simba kwa miaka miwili, raia wa Zambia, Rally Bwalya, amesema kuwa kucheza kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini na klabu ya Amazulu FC ni kutimiza ndoto ambayo alikuwa nayo muda mrefu.

Bwalya alisema kuwa Amazulu ni moja kati ya timu kubwa Afrika Kusini na anaamini itakuwa sehemu ya yeye kuelekea kukua zaidi kisoka na kuipa mafanikio klabu hiyo na yeye kupata mafanikio binafsi.

“Kujiunga na Amazulu kwangu ni mafanikio makubwa kwani nimekuwa nikiitazama na kuifuatilia kwa muda mrefu Amazulu inajulikana sana kwetu Zambia kwa sababu watu wengi wanatazama PSL.

“Ni timu ambayo siyo mpya kwangu, jambo kubwa ni kuisaidia klabu yangu kwa jitihada zote kwani kila mchezaji anakuwa na malengo yake na kuisaidia klabu kufikia malengo yaliyowekwa kwa msimu husika,” alisema.

Bwalya aliagwa wiki iliyopita na Simba na amesaini mkataba wa miaka miwili kukipiga kwenye timu hiyo kutoka katika Mji wa Durban.

BAADA YA FUJO ZA YANGA JANA….WACHEZAJI , MANARA NA SENZO WALIAMSHA KIMTINDO… BAADA YA KUSAJILIWA KWA MBWEMBWE…STRAIKA MPYA YANGA AIBUKA NA KUWEKA HADHARANI MAMBO HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply