Home BIashara United BAADA YA KUTAMBA MISIMU MIWILI LIGI KUU..HIVI NDIVYO BIASHARA UTD INAVYOENDA KUFA…WACHEZAJI...

BAADA YA KUTAMBA MISIMU MIWILI LIGI KUU..HIVI NDIVYO BIASHARA UTD INAVYOENDA KUFA…WACHEZAJI WAIKIMBIA…


Siku chache baada ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kuifungia Biashara United kufanya usajili katika madirisha mawili ya uhamisho wa wachezaji mfululizo, mastaa wa timu hiyo wameanza kuagana kimya kimya na huenda wakaondoka mwisho wa msimu huu.

Tarifa za kuaminika zinadai kuwa ukiachana na adhabu ya kufungiwa usajili, mwenendo mbovu wa timu hiyo kwa msimu huu na madai ya stahiki za wachezaji ni kati ya sababu zinazowafanya mastaa hao kutaka kuondoka kikosini hapo.

Biashara ipo nafasi ya 14 na pointi 28 ikihaha kutoshuka daraja ikiwa imesaliwa na mechi moja dhidi ya Azam ambayo hata ikishinda itaishia kucheza mechi za mtoano ‘playoff’ ili kuwania nafasi ya kubaki kwenye ligi.

“Hii timu inaenda kufa, matatizo yanaiandama wakati ambao ipo katika nafasi mbaya kwenye ligi. karibu kila mchezaji anaidai, ndio hivyo tena imefungiwa kusajili yaani hapa kila mtu haelewi,” alisema kigogo mmoja aliyeomba jina lake kuhifadhiwa na kuongeza;

“Wachezaji wameanza kuagana, msimu ujao tunaweza tusiwe na asilimia 90 ya wachezaji tulionao msimu huu, na kikubwa kinachowaondoa ni hali ya uchumi ya timu na wengine wamepata malisho bora kuliko hapa. Tunasubiri ligi imalizike tuone itakuwaje.”

Wanaotarajiwa kusepa ni Ramadhan Chombo, Abdulmajid Mangalo, Daniel Mgore, Deogratius Judika, Lenny Kissu, James Ssetuba, Opare Collins na Stephen Zigah.

SOMA NA HII  ONYANGO...NDIYO HIVYO TENA. SIMBA....MECHI MOJA TU YANGA..KWISHA KAZI...| MwanaSport

1 COMMENT

  1. I believe everything said was actually very logical.
    But, what about this? what if you added a little information?
    I ain’t suggesting your content is not solid, however what if
    you added a title to maybe get a person’s attention? I mean BAADA YA KUTAMBA MISIMU MIWILI LIGI KUU..HIVI NDIVYO BIASHARA UTD INAVYOENDA
    KUFA…WACHEZAJI WAIKIMBIA… | Soka La Bongo is kinda
    plain. You should look at Yahoo’s home page and watch how they create article titles to
    get viewers interested. You might add a video or
    a related picture or two to get people interested about everything’ve written. In my opinion, it would bring your blog a
    little livelier.

    Also visit my web page: Bonus New Member