Home Azam FC AZAM FC WAJIBU MAPIGO KWA SIMBA NA YANGA…WASHUSHA KINDA LA TIMU YA...

AZAM FC WAJIBU MAPIGO KWA SIMBA NA YANGA…WASHUSHA KINDA LA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST..NI BALAA NA NUSU…

[the_ad id="25893"]


Klabu ya Azam FC imekamilisha Usajili wa Kiungo Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Junior Kwa mkataba wa miaka mitatu.

Staa huyo ambaye jina lake kamili ni Kipre Junior Zunon Tiagouri Emmanuel, amenunuliwa na Azam FC kutokea timu ya Sol FC ya kwao,Na pichani akisaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa (@yusufbakhresa) na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin (@abdulkarim.amin).

Nyota huyo aliyekuwemo kwenye kikosi bora cha msimu huu wa Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1), amewahi kusajiliwa na miamba ya Ufaransa, Strarsbourg msimu wa 2017-2018.

Kiungo huyo mshambuliaji, 22, mwenye kipaji cha hali ya juu pia aliwahi kuwatumikia vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosas, 2018-2020.

Ubora wake ulimfanya pia kuchezea timu za Taifa za vijana za Ivory Coast U-15 na U-17, pamoja na kikosi cha wachezaji wa ndani (CHAN) 2020.

SOMA NA HII  MWARAMU NA WENZAKE KUNZA KUANIKA UKWELI WOTE MAHAKAMANI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here