Home Habari za michezo DK MWIGULU AMPAISHA MAYELE BUNGENI….GSM YAMWAGIWA SIFA KWA KURUDISHA FURAHA YANGA…

DK MWIGULU AMPAISHA MAYELE BUNGENI….GSM YAMWAGIWA SIFA KWA KURUDISHA FURAHA YANGA…


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewatupia dongo mashabiki wa Klabu ya Simba nchini huku akimsifia mchezaji wa Yanga raia wa Congo DR, Fiston Kalala Mayele kuwa mchezaji huyo anafanya nchini vizuri na amekuwa maarufu kuliko hata baadhi ya viongozi.

Mwigulu ambaye ni shabiki kindakindaki wa Yanga amesema hayo leo, Jumanne, Juni 14, 2022 wakati akimalizia kuwasilisha hoja ya mapendekezo ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 Bungeni jijini Dodoma.

“Nakupongeza Mheshimiwa Anthony Mavunde wewe ndio ulikuwa Mwenyekiti wa kuisaidia Yanga ikiwa na mapito. Nampongeza GSM kwa kurejesha furaha ya wananchi hasahasa kwa udajili wa Fiston Mayele.

“Mayele amekuwa maarufu kuliko Makatibu wenezi wa baadhi ya vyama vya Siasa. Nawapongeza sana na marafiki zangu klabu ya Simba kwa kuwakilisha vyema kwenye mashindano ya Kimataifa, wananijua mara zote kimataifa tuko pamoja, siwezi kukana Bendera ya Taifa langu kwa ajili ya utani wa jadi,” amesema Mwigulu.

Ikumbukwe kuwa, Mayele ndiye mchezaji mwenye mabao mengi kwa sasa kwa wachezaji wa Yanga lakini anashika nafasi ya pili kwa wafungaji wa Ligi Kuu mpaka sasa akiwa na jumla ya mabao 14 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na George Mpole wa Geita Golf FC mwenye mabao 15.

Wawili hao ndio wanatajwa kuwania kiatu cha ufungaji Bora wa Msimu wa 2021/2022 ambayo bado mizunguko mine ili kutamatika kwa ligi hiyo ambapo Yanga wanahitaji pointi tatu tu kutangaza ubingwa huku wakiwa na mechi nne mkononi mpaka sasa.

SOMA NA HII  WAZUNGU WALIOLETWA NA SIMBA BONGO WAANZA NA MZIZE....SILI LAKE LAPELEKWA KIMYA KIMYA..