Home Habari za michezo GOLI ALILOIFUNGA SIMBA LAZIDI KUMGANDA KIIZA…AFUNGUKA HALI ANAYOPITIA TOKA AFUNGE GOLI HILO…

GOLI ALILOIFUNGA SIMBA LAZIDI KUMGANDA KIIZA…AFUNGUKA HALI ANAYOPITIA TOKA AFUNGE GOLI HILO…

Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Hamis Kiiza ‘Diego’ amesema licha ya kutofanya vizuri kipindi cha hivi karibuni, lakini mashabiki wake wanapaswa kuendelea kumuunga mkono kwani bila wao sio chochote.

Akizungumza juzi, Kiiza alisema sababu kubwa ya kutofunga kwa muda mrefu ni kutokana na ushindani uliopo ila kila anapopata nafasi anahakikisha anaiwezesha timu yake kupata matokeo chanya.

“Suala la kutokufunga linamtokea kila mtu lakini haina maana huchezi vizuri, bado ukiangalia kwa jinsi ninavyocheza hapa siwezi kujiangalia mimi binafsi, bali timu kwa ujumla ingawa kazi ya mshambuliaji ni kufunga,” alisema.

Kiiza alieleza kuwa licha ya kutokuwa kwenye sehemu ya kikosi cha kwanza mara kwa mara, ila hilo kwake sio tatizo kwani kocha ndiye anayeamua wa kumuanzisha kutokana na mchezo husika na mahitaji ya timu.

“Kwanza nafurahi kwa sababu ya heshima ninayoipata hapa ukiangalia ningekuwa timu nyingine na vijana wanapata nafasi zaidi yangu wangeanza kunidharau ila hilo halipo jambo ambalo najivunia kufanya nao kazi.”

Nyota huyo wa zamani wa Simba na Yanga tangu ajiunge na timu hiyo Januari, mwaka huu amefunga bao moja tu kwenye ushindi wa 1-0, dhidi ya Simba Januari 26 na hadi sasa katimiza siku 145 bila kufunga sawa na saa 3,480.

SOMA NA HII  KIUNGO HUYU YANGA NDIO BASI TENA...AFANYIWA UPASUAJI WA GOTI....KUIKOSA MECHI NA SIMBA