Home Habari za michezo KIBU DENIS AKINGIWA KIFUA MSIMBAZI…KASONGO AWAPA ZA USO MABOSI SIMBA KUHUSU USAJILI...

KIBU DENIS AKINGIWA KIFUA MSIMBAZI…KASONGO AWAPA ZA USO MABOSI SIMBA KUHUSU USAJILI MPYA…


BEKI wa zamani wa Simba, Kasongo Athumani  anaamini endapo straika wa timu hiyo, Kibu Denis akivumiliwa msimu ujao atafanya makubwa.

Amezungumza jana Alhamisi ya Juni 9, 2022  kwa njia ya simu, kwamba Kibu ni straika mzuri,  ila ameingia Simba akiwa na changamoto nyingi zilizochangia asianze kwa kishindo.

“Simba wakati inamsajili Kibu kutoka Mbeya City, kulikuwa na mambo mengi, sasa mchezaji ili afanye vizuri anategemea utulivu, soka linahitaji kutumia maarifa mengi, kuliko nguvu bila akili,” amesema na kuongeza;

“Ndio maana Kibu ameanza kuonyesha makali yake mechi za mwishoni, maana yake akili yake imeanza kutulia, binafsi naona ana vitu vingi mguuni kwake.

Amesema wakati Simba inakwenda kufanya marekebisho baadhi ya nafasi, anaishauri kamati ya usajili itulize akili kufanya maamuzi sahihi.

“Ndio maana nimesema mchezaji kama Kibu wanapaswa kumpa nafasi, maana huwezi kupangua timu nzima,” amesema.

SOMA NA HII  Furahia Book of Egypt, Sloti Mpya Kabisa kwa Ajili Yako

1 COMMENT

  1. KUTOKA KUWA MKIMBIZI MPAKA KUSAJILIWA SIMBA SC….HAYA NDIO MAPITIO HALISI YA KIBU DENIS… - Bongo Soka

    […] na kule msimu ukaisha na kuanza msimu huu na Kibu hali ikazidi kumweka ngumu ndani ya Simba lakini akaamini katika mchakato na kukaza […]