Home CAF KUHUSU MASHINDANO YA CAF MSIMU UJAO NA TAREHE RASMI YA KUANZA..UKWELI WOTE...

KUHUSU MASHINDANO YA CAF MSIMU UJAO NA TAREHE RASMI YA KUANZA..UKWELI WOTE HUU HAPA…


Hatimaye Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limetangaza tarehe ya kuanza kwa Michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa msimu ujao 2022/23.

‘CAF’ imetoa taarifa hizo kupitia ‘Caf Online’ ambapo imethibitika kuwa, hatua ya awali ya michuano hiyo mikubwa Barani Afrika upande wa vilabu, itaanza rasmi siku ya Ijumaa (Agosti 12).

Hatua ya makundi ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho itanza mwezi Septemba na kumalizika Novemba 18-2022

Hatua ya Mtoano katika michuano hiyo imepangwa kuanza Mwezi Februari-2023, baada ya kumalizika kwa Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN 2023’ zitakazounguruma nchini Algeria.

Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na timu nne katika michuano ya CAF upande wa vilabu msimu ujao, ambapo Ligi ya Mabingwa kuna dalili miamba ya Simba SC na Young Africans ikashiriki, huku upande wa Kombe la Shirikisho, ikiwa bado haijafahamika hadi sasa ni timu zipi zitakata tiketi ya michuano hiyo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA SIMBA KAMA WAMEMCHUNIA HIVI...ADEBAYOR AWAPIGIA MAGOTI WAMSAJILI...