Home Habari za michezo MAMBO YAZIDI KUFICHUKA SAKATA LA PABLO KUFUKUZWA SIMBA….KUMBE UGOMZI WAKE NA CHAMA...

MAMBO YAZIDI KUFICHUKA SAKATA LA PABLO KUFUKUZWA SIMBA….KUMBE UGOMZI WAKE NA CHAMA ULIPELEKEA YOTE HAYA…


Imebainika Kuwa kumbe kitendo cha kutimliwa kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ni pamoja na kumuondoa kwake kambini jijini Mwanza, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Zambia Cloutas Chama.

Mmoja wa Wajumbe wa kamati ya usajili ya Simba, KD’’ amesema kuwa Pablo hakumpenda Chama tangu anaingia kikosini hapo kwakuwa hakuwa sehemu ya mipngo ya usajili wake kwenye dirisha dogo, hali hiyo ilimfanyav kujenga chuki kwa Chama kiasi cha kupelekea kugombana mara kadhaa kila Chama aliposhauri jambo hata jema.

Mbali na hivyo utaona Chama alitimuliwa kwenye kambi ya maandalizi ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports, jijini Mwanza jambo lililomfanya Chama kutimkia kwao Zambia.

Lakini kama hiyo haitoshi, kwenye mechi ya Ligi dhidi ya Yanga, wawili hao walionekana kuzozana, ambapo Pablo hakufurahishwa na kiwango cha uchezaji wa Chama kwenye mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa sare.

Pia, Kwenye mechi dhidi ya Polisi Tanzania Mkoani Kilimanjaro, Pablo aliamua kutomtumia Chama pamoja na kuwa hakuwa majeruhi kama ilivyosasa, huku nnje ya Uwanja mabosi wa Simba wakiuaminisha umma wa mashabiki zao kuwa kiungo huyo raia wa Zambia ni Majeruhi.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE