Home Habari za michezo MFAHAMU KOCHA MPYA SIMBA…ANAUZOEFU NA SOKA LA AFRIKA KWA MIAKA 10…AMESHINDA LIGI...

MFAHAMU KOCHA MPYA SIMBA…ANAUZOEFU NA SOKA LA AFRIKA KWA MIAKA 10…AMESHINDA LIGI YA ANGOLA NA ALGERIA TU..


Klabu ya Simba siku ya jana ilimtambulisha Zoran Maki Manojlovi, raia wa Serbia kuwa kocha wao mkuu ambaye anakuja kurithi mikoba ya Pablo Franco Martin ambaye alitimuliwa kwenye klabu hiyo kufutai matokeo mabovu.

Kocha huyo amepewa mkataba wa mwaka mmoja, ambaye atajiunga na timu hiyo katika maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2022/23, ambao unatarajia kuanza Tarehe 17 Agosti 2022.

Zoran ni moja ya kocha mwenye uzoefu na soka la bara Afrika, mara baada ya kuhudumu ndani ya mabara hili katika kipindi cha miaka 10 na kupata mafanikio tofauti.

Ikukumbukwe kabla ya mchakato kuanza wa kumtafuta kocha ndani ya klabu ya Simba, uongozi wa timu hiyo uliweka bayana kuwa kocha watakayemuhitaji ni yule ambaye analijua vizuri soka la abarani Afrika.

Mafaniko makubwa ya kocha huyo ndani ya bara Afrika, alifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu nchini Angola msimu wa 2018/19, akiwa na klabu ya De Agosto ambayo pia alifanikiwa kuifikisha hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Aidha pia Zoran alifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Algeria akiwa na Klabu ya Belouzdad msimu wa 2020/21, lakini pia naliwahi kuvifundisha klabu za Wydad Casablanca ya Misri (2019/20) De Agosto ya Angola (2018/19) Al hilal ya Sudan (2020/21) na Vila real (2006).

SOMA NA HII  MASTAA HAWA 10 WA SIMBA KUIKOSA MECHI YA KENYA