Home Habari za michezo NAMUNGO vs YANGA VIINGILIO HADHRANI, MAMBO YAPO HIVI

NAMUNGO vs YANGA VIINGILIO HADHRANI, MAMBO YAPO HIVI

Habari za Yanga

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumatano, Septemba 20 katika uwanja wa Azam Complex

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Kamwe alitangaza kuwa mchezo huo watautumia kuwaenzi mashabiki waliosafiri kwa wingi kwenda Rwanda kuishangilia Yanga kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

Kamwe alitangaza viingilio vya mchezo huo ambapo VIP A ni Tsh 20,000/-, VIP B ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000.

“Yanga imekuwa klabu ya kwanza barani Afrika kusafiri na mashabiki wengi katika mechi ya ugenini na kujaza uwanja. Hili ni jambo lililotupa heshima kubwa Afrika nzima na hivyo tumeufanya mchezo dhidi ya Namungo Fc kuwa maalum kwa ajili ya mashabiki waliosafiri Rwanda.

“Tumeandaa utaratibu siku ya Jumatano ambapo itakapofika dakika ya 12 mashabiki wote watasimama na kupiga makofi kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kuwapongeza wote waliosafiri na timu Rwanda.

“Uongozi pia umeandaa surprise kwenye dakika ya 12 ambayo itaonekana uwanjani na Azam Tv kwa wale ambao hawatakuwa uwanjani. Tunawaomba hata wale ambao watakuwa nyumbani au katika vibanda umiza wasimame kwenye dakika ya 12 kuwapa maua yao wale waliosafiri Rwanda,” alisema Kamwe

SOMA NA HII  VIJANA WA SIMBA WALIOIPA TABU AL AHLY WASEPA JUMLAJUMLA