Home Habari za michezo MORRISON AFUATA NYAYO ZA OKWI SIMBA NA YANGA….ACHOTA MAMILIONI YA PESA PANDE...

MORRISON AFUATA NYAYO ZA OKWI SIMBA NA YANGA….ACHOTA MAMILIONI YA PESA PANDE ZOTE KIULAINII…


Kila kona kwa sasa kwenye soka la Bongo ni ‘saga’ la winga raia Ghana, Benard Morrison, ambaye ameoneyeshwa mkono wa kwaheri na Simba, lakini kuna tetesi kuwa anaweza kurejea Yanga alipotoka misimu miwili iliyopita.

Morrison ameiteka mitandao na vijiwe tofauti tofauti kitaa kuhusu ishu yake na kubwa zaidi ni kutokana na vituko vyake alivyovifanya akiwa ndani ya timu hizo mbili kubwa kwenye soka hapa nchini.

Liakini wala jambo hilo sio jipya masikioni au machoni kwa wadau wa soka nchini kwani jambo las kutoka pande moja (Simba na Yanga) na kwenda pande nyingine kisha kurudi bila kujali nini kilitokea mwanzo lishafanya na mastaa kibao na bado maisha yakaendelea.

Kupitia makala hii, Gazeti la Mwanaspoti linakuletea baadhi ya matukio tata yaliyotokea kwa uhamisho wa wachezajizi ukizihusisha Simba na Yanga ambazo zinaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini na wenye mapenzi, machungu na hisia kali juu ya tumu hizo.

Bernard Morrison

Ni winga ambaye alitua nchini kipindi cha dirisha dogo la usajili msimu wa 2019/20 na klabu ya Yanga ambayo aliitumikia kwa miezi sita na baadaye kutimkia Simba usajili wake ambao ulikuwa na utata mkubwa na kesi Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS)

Usajili wake kwenda Simba ulishtua sana kutokana na uwezo wake ukubwa aliounyesha ndani ya Yanga ndani ya miezi sita aliyopata nafasi ya kucheza na baadaye ikatoka tarifa ya kutua upande wa pili mashabiki wa Yanga hawakutaka kukubaliana na hilo baada ya kuaminishwa kuwa staa huyo alisainishwa kwa mkataba wa miaka miwili kumbe sio kweli.

Haruna Niyonzima

Kiungo huyo mzaliwa wa Gisenyi nchini Rwanda. ni miongoni mwa wachezaji ambao usajili wao ulitikisa kutokana na ukubwa wake na kiwango alichokuwa nacho kwa wakati huo. Baada ya kuitumikia Yanga kwa misimu saba akitokea APR ya Rwanda msimu wa 2011, Niyonzima alisepa zake Simba, msimu wa 2019, Niyonzima aliisaidia Simba kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoa pasi ya mwisho ya bao Clatous Chama lililopelekea Simba kutinga hatua hiyo. Baada ya kuitumikia Simba misimu miwili nyota huypo wa zamani wa Rayom Sports alirejea Yanga.

Amis Tambwe

Mrundi huyu alisaini Simba 2013 baada ya kuibuka mfungaji bora Kombe la Kagame, alitupiwa vilago ndani ya Simba baada ya kudumu kwa msimu mmoja licha ya kuibuka kinara wa mabao Ligi Kuu, alitua Yanga 2014 na kufanikiwa kuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya kikosi baada ya kufanikiwa kufunga mabao zaidi ya 70 katika mashindano yote, kadhalika kuisaidia klabu kushinda mataji mbalimbali.

SOMA NA HII  MZAMIRU AANIKA SIRI ZAKE SIMBA...AFUNGUKA ISHU YA MKUDE KUPIGWA BENCHI HUKU YEYE AKIANZA...

Ni usajili ambao Simba ilijutia kumwacha Tambwe na kumpeleka kwa watani zao, Yanga kutokana na rekodi zake kuwa wazi tangu alipojiunga na Yanga.

Hamis Kiiza

Kiiza maarufu kama Diego, Mganda huyu mwenye rekodi nzuri ya ufungaji kwasasa anakipiga Kagera Sugar alifukuzwa na Yanga na kuja kuibuka shujaa ndani ya Simba.

Usajili wake ndani ya Simba ulisambaa akiwa njini kwao kwenye ukumbi wa harusi ya mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ambapo baada ya kuulizwa swali na mwandishi kuhusu soka alimjibu kuwa atarudi tena Tanzania kuitumikia Simba.

Emmanuel Okwi

Hakuna aliyeamini aliposikia Okwi anatua Tanzania kwa ajili ya kuitumikia Yanga, lakini ilifanikiwa na mshambuliaji huyo mwenye mapenzi na Simba aliitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Usajili huo uliwastua mahasimu wao, Simba ambao walikuwa na mgogoro na mchezaji huyo na klabu waliyomuuza ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya Dola 300,000 (Sh 480 milioni).

Hata hivyo wakati Simba wakiwa katika mgogoro huo, Yanga waliibuka na kumsajili mchezaji huyo saa chache kabla ya muda uliowekwa na TFF kwa klabu kukamilisha usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu Bara.

Klabu zote za Ligi Kuu zilitakiwa kufanya kusajili wa wachezaji wapya kuanzia Novemba 15/ hadi Desemba 15 saa sita usiku 2013.

Okwi kwa mara ya kwanza alisajiliwa na Simba 2010 akitokea Sports Club Villa ya Uganda, kabla ya kumuuza Etoile du Sahel, tangu Simba imuuze suala la malipo lilikuwa gumu, huku Okwi akilalamika kuidai klabu hiyo haimlipi mshahara na marupurupu.

Kutokana na hali hiyo alikubali kusaini SC Villa mkataba wa miezi sita baada ya klabu hiyo kuomba kibali maalumu Fifa ili kumtumia kwa lengo kuokoa kipaji chake jambo ambalo viongozi wa Simba walilipinga na kuahidi kulikatia rufaa Fifa.

Desemba 2013, Yanga wakatangaza kumsajili Okwi kutoka Sports Club Villa ya Uganda. Usajili huo ukazua utata uliopelekea TFF kusitisha usajili wake na kuomba ufafanuzi FIFA kuhusu uhalali wa usajili wa mchezaji huyo.