Home Uncategorized MANCHESTER UNITED WAINGIA KWENYE VITA NA BARCELONA,PSG KUISAKA SAINI YA AUBA

MANCHESTER UNITED WAINGIA KWENYE VITA NA BARCELONA,PSG KUISAKA SAINI YA AUBA


 MANCHESTER United imeweka mezani pauni milioni 50 ili kuinasa saini ya nyota wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang.

Imeelezwa kuwa Auba amekuwa kwenye hesabu ya timu kubwa zinazotaka saini yake kwa sasa ikiwa ni pamoja na Barcelona, PSG ambazo zimeonesha nia ya kuitaka saini yake.

Arsenal wapo tayari kumuweka Auba sokoni ili kupata mkwanja mrefu nyota huyo ambaye dili lake linakaribia kumeguka ndani ya Arsenal na hajaongeza mkataba mwingine.

Kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya Arsenal na Auba kuhusu mkataba wa nyota huyo mwenye miaka 30.

Iwapo hatasaini mkataba mpya kwa sasa anaweza kuondoka bure ndani ya Arsenal iliyo chini ya Mikel Arteta.

SOMA NA HII  WACHEZAJI SABA WA SIMBA WANAOPEWA NAFASI YA KUSEPA MSIMU UJAO