Cristiano Ronaldo ameomba kuondoka Manchester United ambapo inadaiwa lengo lake ni kuendelea kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya taarifa kuwafikia baadhi ya mashabiki wa timu yake wakasema โmuacheni aendeโ
United haijafuzu katika ligi hiyo badala yake itashiriki Europa League. Sababu nyingine inayotajwa kumuondoa Ronaldo (37) ni United kushindwa kufanya usajili mzuri kwa ajili ya msimu ujao.
Baadhi ya mashabiki wa United wametumia mitandao ya kijamii kusema klabu imruhusu aondoke. Anatajwa kuwaniwa na Chelsea na Bayern Munich.