Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO…MTIBWA SUGAR WASHTUKA JAMBO…WAANZA KUTEMBEA NA ‘BITI’ LA SIMBA NA...

KUELEKEA MSIMU UJAO…MTIBWA SUGAR WASHTUKA JAMBO…WAANZA KUTEMBEA NA ‘BITI’ LA SIMBA NA YANGA…


Baada ya kuusotea ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa zaidi ya miaka 22, klabu ya Mtibwa Sugar, imepanga kufanya usajili wa kuhusisha nyota wa kigeni, ili waipige tafu ikiziiga Simba, Yanga na Azam ambazo zimekuwa zikibebwa zaidi na wageni

Mabosi wa klabu hiyo ya Manungu ambayo ni kati ya timu ambazo tangu zipande daraja hazijawahi kushuka Ligi Kuu, wamebaini kutegemea wazawa pekee yake katika soka la ushindani lililopo sasa kunawachelewesha na sasa wameamua kuiga wakubwa wenzao.

Mtibwa kwa sasa inawamiliki wageni wanne Boban Zirintusa na Brian Mayanja kutoka Uganda, Styve Nzigamasabo wa Burundi na Mkongomani, Deo Kanda , ambao waliipigania timu na kuinusuru isalie kwa msimu ujao kwa play-off.

Za Ndaaani Kabisa zinasema kuwa, Mtibwa sasa inarudi kuwajaza wageni ili waipiganie na kubeba ubingwa baada ya kuupata mara ya mwisho mwaka 2000 walipoutetea kwa mara ya pili, ikiwa na kocha mzawa, John Simkoko.

“Baada ya Azam Media kuweka mzigo wa maana kwenye ligi, tumeona ni muda wa kubadilika na kusajili wachezaji wa kigeni wenye viwango vya kuipigania timu, tuna hamu na sisi kubeba ubingwa, ligi kwa sasa imekuwa yenye ushindani,” alisema mmoja wa vigogo wa timu hiyo na kuongeza; “Hii hali ya kusubiri hadi dakika ya mwisho kunusurika kushuka daraja, sio afya nzuri kwa timu kubwa kama hii, ngoja tuone.”

SOMA NA HII  AZIZ KI AENDELEA KUMUONYESHA UBABE CHAMA...TFF WATHIBITISHA KWA TAARIFA HII