KIPA namba moja ndani ya kikosi cha Simba, Aishi Manula ameongeza kandarasi ya miaka mitatu kuweza kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo.
Kikawaida imezoeleka wachezaji wa ndani hupewa mikataba mifupi ya miaka miwili au mmoja, lakini Manula ameweza kuushawishi uongozi wa Simba kumpa mkataba mrefu wa miaka mitatu kama zifanyavyo timu za Ulaya.
Inaelezwa kuwa mkataba huo wenye thamani ya Milioni mia tatu, utamfanya Manula kuwa miongoni mwa wachezaji ghali zaidi nchini, ambapo ikitajawa kuwa kwa mwezi atakuwa akilipwa Milioni kumi nnje ya posho na marupurupu mengine.
Awali nyota huyo alikuwa anatajwa kuingia anga za Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na kulikuwa na mazungumzo na timu mbalimli.
Kipa huyo ni chaguo la kwanza ndani ya Simba ambapo kwa sasa yupo kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo inajiandaa kufuzu CHAN.
Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Simba leo Julai 20,2022 imeeleza kuwa Manula bado yupo ndani ya Simba kwa msimu mitatu mpaka 2025.