Home Habari za michezo BAADA YA KUONA ISHU YA KAMBI KAMA INAMCHANGANYA…NABI AIBUKA NA MAAMUZI HAYA...

BAADA YA KUONA ISHU YA KAMBI KAMA INAMCHANGANYA…NABI AIBUKA NA MAAMUZI HAYA MAGUMU KWA YANGA…


Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Nabi, amesema hana shaka na Kambi ya kikosi chake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Young Africans ilitarajiwa kuanza Kambi mwishoni mwa juma lililopita, lakini hadi sasa haijaanza Kambi ya Maandalizi yake, hali ambayo inazua hofu kwa Mashabiki na Wanachama wake.

Kocha Nabi amesema Uongozi wa juu unashughulikia Kambi ya kikosi chake, na hana wasiwasi na hilo, kutokana na kuamini muda bado upo wa kufanya Maandalizi ya kutosha.

Amesema anaamini Mashabiki na Wanachama wana hamu ya kufahamu wapi timu yao itakapoweka Kambi, lakini kwake kama Mkuu wa Benchi la Ufundi hana haraka na suala hilo, ambalo ana uhakika litafanyika kwa wakati.

“Nafikiri suala la wapi tutaweka kambi hilo linafanyiwa kazi na viongozi naona kama watu wamekuwa na wasiwasi kutokana na kile kilitokea huko nyuma,”

“Tuna muda bado, wiki hii wachezaji wanamalizia mapumziko, sidhani kama tumechelewa sana labda watu wana kiu ya kutaka kujua wapi tutakwenda.”

“Kama itaamuliwa wiki inayoanza leo haitakuwa mbaya kwa kuwa hata wachezaji mapumziko yao yanaisha wiki hii, kama tukipata wiki tatu tutakuwa tumefanikiwa sana.” amesema Kocha Nabi

Wakati Kocha Nabi akiwa na uhakika wa kuanza kwa Kambi ya kikosi chake wakati wowote kuanzia sasa, Simba SC imeshaanza Kambi ya Maandalizi ya msimu ujao nchini Misri na jana Jumapili (Julai 17), ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ismailia na kuambulia sare ya 1-1.

Young Africans itacheza dhidi ya Simba SC katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii Agosti 13, ikiwa ni kiashirio cha kufunguliwa rasmi kwa msimu mpya wa 2022/23.

SOMA NA HII  ASEC WATUA NCHINI KUWAKABILI SIMBA