Home Habari za michezo BAADA YA KUWA NAYE KWA MSIMU MMOJA….KMC WAAMUA LIWALO NA LIWE KWA...

BAADA YA KUWA NAYE KWA MSIMU MMOJA….KMC WAAMUA LIWALO NA LIWE KWA HASSAN KESSY….’WAMTUPIA VIRAGO’….

[the_ad id="25893"]


Klabu ya KMC imeachana na aliyekuwa beki wake, Hassan Kessy baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja wa kuwatumikia kufikia ukomo.

Kessy alijiunga na KMC Septemba Mosi 2021 kwa kandarasi ya mwaka mmoja akitokea klabu ya Mtibwa Sugar baada ya kushindwa kufikiana maslahi binafsi huku nafasi yake ikichukuliwa na aliyekuwa staa wa Coastal Union, Hassan Kibailo.

Beki huyo alijiunga na KMC kwa ajili ya kuziba pengo la aliyekuwa nyota wa kikosi hicho, Israel Mwenda aliyejiunga na Simba.

Kabla ya kurejea nchini Kessy alikuwa akiichezea Nkana ya Zambia aliyojiunga nayo 2018 akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara Yanga.

Timu alizowahi kuchezea nyota huyo ni pamoja na Mtibwa Sugar 2011-14, Simba 2014-16, Yanga 2016-18 kisha kutimkia Nkana 2018 na kurudi tena hapa Tanzania.

SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA HAKUNA MBABE...TAMBO ZIMEISHA MIDOMONI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here