Home Habari za michezo BAADA YA SOPU NA AKPAN KUSEPA…COASTAL UNION WAJIBU MASHAMBULIZI…WAANZA NA BEKI KITASA...

BAADA YA SOPU NA AKPAN KUSEPA…COASTAL UNION WAJIBU MASHAMBULIZI…WAANZA NA BEKI KITASA WA SIMBA…


BAADA ya Simba kutajwa imemchukua kiungo mkabaji wao raia wa Nigeria, Victor Akpan,  Coastal Union inadaiwa iko katika mazungumzo na beki wa kati wa timu hiyo, Kennedy Juma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Coastal Union, Ahmed Aurora alisema jana tayari wameshaanza usajili, lakini wao siyo kama timu nyingine zinazotangaza kila hatua waliyofikia, bali wao wanasajili kimya kimya na kwa umakini bila kukurupuka.

Aurora alisema baada ya Abdul Suleimani ‘Sopu’ aliyejiunga na Azam na Akpan ambaye ameshasaini Simba, nao wameingia katika kinyang’anyiro cha usajili kwa ajili ya kuitengeneza Coastal Union iwe nzuri zaidi kuliko ya msimu uliopita.

Mbali na Kennedy, Coastal Union inatajwa kumwania straika wa Mtibwa Sugar, Jaffar Kibaya pamoja na beki wa kulia wa Prisons, Salum Kimenya.

“Na siyo hao tu peke yao, wapo wengi tumezungumza nao, sitaki kupindisha maneno, ni kweli tunawafuatilia wachezaji wao na kwa asilimia 50 tumemalizana nao, bado tunaendelea asilimia zilizobaki, tukikamilisha tutawatangazia, siku zote sisi hatukurupuki na huwa hatutangazi,” alisema Aurora.

Aliongeza kwa mujibu wa mapendekezo ya benchi la ufundi, maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ni ushambuliaji na mabeki wa pembeni.

SOMA NA HII  BAADA YA KUICHAPA YANGA , RIVER PLATE WAFUNGUKA HUJUMA ZA YANGA..WAITAJA ENYIMBA FC