Home Geita Gold FC BENCHI LAMFANYA MPOLE KUTEMBEA NA MKATABA WA SIMBA KWENYE BEGI….AFUNGUKA HAYA KUHUSU...

BENCHI LAMFANYA MPOLE KUTEMBEA NA MKATABA WA SIMBA KWENYE BEGI….AFUNGUKA HAYA KUHUSU HATMA YAKE….


George Mpole amethibitisha bado hajafahamu atacheza timu gani msimu ujao, huku akizitaja Simba na Geita Gold kama miongoni mwa timu zilizompa ofa nono.

Taarifa za kuaminika zinasema Simba imempa ofa mchezaji huyo lakini amekuwa akijishauri sana na kuishia kutembea na mkataba wao mfukoni jambo ambalo limefanya wafikie uamuzi wa kuachana nae ingawa hawajamwambia rasmi.

Mpole aliyemaliza msimu kwa kutupia mabao 17 alilSEMA ana ofa nne ambazo hadi sasa bado hajazifanyia maamuzi.

Akizungumza Mpole alisema amemaliza mkataba na waajiri wake Geita Gold hivyo kwa sasa ni mchezaji huru na anachosubiri ni kupata ofa sehemu nyingine huku akiweka wazi suala lake amewaachia wasimamizi wake kulishughulikia kabla ya kuanza msimu mpya.

“Nipo Mbeya naendelea na mazoezi binafsi bado sijajua nitacheza timu gani msimu ujao na sipo tayari kulizungumzia hilo kwa sasa kwa sababu nimewaachia wasimamizi wangu na mambo yakiwa tayari kila kitu nitakiweka wazi timu nitakayochezea,” alisema na kuongeza;

“Nataka kwenda kucheza timu ambayo itanipa kipaumbele cha kucheza kikosi cha kwanza ili niweze kuendeleza pale nilipoishia, haitakuwa sawa kwenda sehemu ambayo nitakaa benchi kwani wadau wengi wanatamani kuona mwendelezo wangu mzuri baada ya hiki nilichokifanya msimu ulioisha.”

Mpole alisema mpira ndio kazi yake na hatamani kupoteza uaminifu alioujenga kwamba yeye ni mchezaji mzuri kwenye suala la kufunga hivyo anatamani kucheza timu ambayo ataanza nayo vizuri na kumaliza vizuri.

Mwenyekiti wa Geita Gold, Costantine Morandi alipotafutwa alithibitisha kuwepo kwenye mchakato wa kumbakiza mchezaji huyo; “Tupo kwenye mchakato wa kumbakisha Geita Gold tumempa ofa nyingine kama atashawishika basi ataendelea kubaki na sisi kwa misimu mingine miwili lakini kama atashindwa basi hatutakuwa na namna zaidi ya kusaka mbadala wake,” alisema Costantine.

Geita tayari wameshamalizana na mshambuliaji, Yacouba Sogne kutoka Yanga.

SOMA NA HII  GAMONDI ASHANGAZWA NA MAISHA YA MASTAA YANGA...AMEFUNGUKA HAYA