Home Habari za michezo HUKU AKITAZAMWA NA BARBARA…MAKI APONDA VIWANGO VYA MASTAA WAPYA SIMBA….

HUKU AKITAZAMWA NA BARBARA…MAKI APONDA VIWANGO VYA MASTAA WAPYA SIMBA….


Baada ya kupoteza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Haras El Hodoud ya Misri, jana Jumatano (Julai 27) Kocha Mkuu wa Simba SC Zoran Maki amesema bado kuna kazi ya kufanya kwenye kikosi chake.

Simba SC ipo Kambini mjini Ismailia-Misri, ikijiandaa na Msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika kwa msimu wa 2022/23.

Kocha Zoran amesema baada ya mchezo huo uliopigwa mjini Cairo amebaini kuna changamoto ya kutengeneza nafasi katika eneo la mwisho, hivyo atahakikisha katika kipindi hiki cha kuendelea na Kambi, analimaliza tatizo hilo ambalo pia lilikua sugu msimu uliopita.

Katika hatua nyingine Kocha huyo kutoka nchini Serbia amesema safu ya Kiungo ya Kikosi chake nayo ilikua shida kwenye mchezo huo, hali ambayo ilichangia wapinzani wao kuwashinda kirahidi kwa mabao 2-0.

“Hatukuwa na ubora kwenye safu ya kiungo, hatukutengeneza nafasi, ilikua kiasi kidogo. Uwanja haukuwa mzuri sana lakini hiyo sio sababu ya sisi kutotengeneza nafasi, haukuwa mchezo mzuri tu.” amesema Kocha Zoran

Matokeo hayo yanakua mabaya kwa Simba SC, tangu walipoanza Kambi nchini Misri, kwani waliwahi kupata matokeo ya ushindi wa 6-0 dhidi ya Abou Hamad, yakitanguliwa matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Ismailia FC.

Simba SC leo imefikisha siku yaa 13 tangu ilipoanza Kambi mjini Ismailia-Misri, huku ikitarajia kurejea Dar es salaam Tanzania mwanzoni mwa mwezi Agosti 2022.

Itakaporejea Dar es salaam, Simba SC itacheza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki utakaohitimisha sherehe za Simba Day, mnamo Agosti 08-2022.

Agosti 13 Simba SC itacheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtani wake Young Africans, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

SOMA NA HII  TETESI ZA USAJILI:KISA BOCCO....MNIGERIA AJIVUTA KIAINA MSIMBAZI....AFICHUA DILI LAKE LILIVYO...