Home Habari za michezo KISA SOPU NA AKPAN….COASTAL UNION WAZIKAMUA SIMBA NA AZAM ZAIDI YA MILIONI...

KISA SOPU NA AKPAN….COASTAL UNION WAZIKAMUA SIMBA NA AZAM ZAIDI YA MILIONI MIA MBILI…


DILI la Abdul Suleiman ‘Sopu’ na Victor Akpan limewapa mamilioni Coastal Union ambao wametamba kufanya usajili wa maana msimu ujao.

Kuondoka kwa mastaa wawili ndani ya Coastal Union ambayo imemaliza nafasi ya saba kwenye msimamo msimu huu kumeiingizia Sh 200 milioni timu hiyo.

Pesa hiyo imetokana na timu hiyo kuuza mastaa wake wawili kiungo Akpan ambaye anatajwa kujiunga Simba na Sopu aliyetua Azam FC.

Wawili hao walikuwa na mikataba ya kuendelea kuitumikia timu hiyo msimu ujao hivyo uongozi umefanya biashara na timu tajwa hapo juu ili kukamilisha uhamisho wa mastaa hao.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Coastal Union kimeliambia Mwanaspoti kuwa wamevuna kiasi hicho cha pesa baada ya kukamilisha dili za wachezaji hao. Mbali na pesa hizo za usajili timu hiyo imepata Sh55 milioni kutoka kwa wadhamini wenza wa ligi ambao ni Azam Tv na kufanya wakusanye kitisha cha Sh255 milioni. Uongozi umethibitisha kupata kiasi hicho cha fedha na wataendelea kufanya biashara ya kukuza vipaji.

SOMA NA HII  TAKWIMU HIZI ZINASEMA DABI YA KARIAKOO ILICHEZWA KWA DAKIKA 50 TU