Home Habari za michezo KUFUATIA KUSAJILI MASTAA WENGI WA MAANA….NABI AVUNJA UKIMYA KUHUSU NAFASI YA SURE...

KUFUATIA KUSAJILI MASTAA WENGI WA MAANA….NABI AVUNJA UKIMYA KUHUSU NAFASI YA SURE BOY KIKOSINI….


Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Mohamed Nabi ametuliza hofu kwenye kikosi chake, kufuatia usajili wa baadhi ya wachezaji, ambao unaonekana kutishia nafasi za walioitumikia klabu hiyo msimu uliopita na kupata mafanikio.

Young Africans imemsajili Mshambuliaji Lazarius Kambole kutoka Zambia, Beki wa Kushoto Joyce Lomalisa (DR Congo), Kiungo Gael Bigirimana (Burundi) na Kiungo Mshambulijai Bernard Morrison (Ghana).

Usajili huyo umekua gumzo na kuibua maswali kwa wadau wa soka la Bongo, ambao wanahoji uhakika wa kuendelea kutumika kwa baadhi ya wachezaji ambao walikua wakicheza nafasi wanazocheza wachezaji waliosajiliwa katika Kipindi hiki.

Kocha Nabi ambaye kwa sasa yupo Mapumzikoni amesema kila mchezaji aliye kwenye kikosi cha Young Africans ana nafasi ya kuitumikia klabu hiyo, hivyo haoni sababu kwa baadhi yao kuingiwa hofu.

Amesema wachezaji wapya na wale wa zamani klabuni hapo, wote wana viwango bora kikubwa kila mmoja anahitajika kumshawishi mazoezini kwa kuonesha uwezo utakaomuingiza kwenye kikosi cha kwanza.

“Ujio wa wachezaji wapya hauna madhara yoyote kwenye kikosi changu, kila mmoja ana nafasi ya kuwa huru na kuonyesha uwezo wake, ili nimtumie kwenye kikosi cha kwanza, kwa asilimi 100 wote ni bora”

“Nilitoa muda kuangalia uwezo na ubora wa kila mchezaji wangu mazoezini kabla ya kumtumia katika michezo ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ msimu uliopita, hivyo hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa msimu ujao,”

“Najua kuna wachezaji kama Kibwana Shomari, na Sure Boy wanatajwa kama wameshapoteza nafasi zao, kufuatia uwepo wa Bigirimana na Lomalisa, lakini niwahakikishie wote wana nafasi sawa, kazi iliopo ni wao kunihakikishia wana uwezo wa kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza msimu ujao.” Amesema Kocha Nabi.

Kikosi cha Young Africans kinatarajia kuingia kambini leo Alhamis (Julai 14) Avic Town Kigamboni, tayari kwa safari ya kuelekea nchini Uturuki, ambapo kitaweka kambi ya majuma mawili kabla ya kurejea nchini kwa mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 13 dhidi ya Simba SC.

SOMA NA HII  SURE BOY, NKANE RASMI YANGA..NABI AMTEGA MAKAMBO...BWALYA, MORRISON WASHTUA SIMBA...