Home Habari za michezo KUTOKA MISRI….KWA SOKA HILI LA SIMBA…MTU AKIPIGWA CHACHE SANA SANA GOLI TATU…ISHU...

KUTOKA MISRI….KWA SOKA HILI LA SIMBA…MTU AKIPIGWA CHACHE SANA SANA GOLI TATU…ISHU YA KANOUTE IKO HIVI KUMBE…


Dhamira ya Simba kufanya mauaji msimu huu imeanza kuonekana kambini Misri ambako imempiga mtu mabao 6-0 na huku ikileta mabao ya kutosha kwa kusajili washambuliaji wa hatari.

Katika maandalizi ya msimu ujao nchini Misri Simba imeonekana ikicheza kwa kujiamini huku mastaa wake wakitandaza pasi nyingi uwanjani.

Simba inaonekana kuwa na hasira baada ya msimu uliopita kukosa mataji matatu, yakienda kwa watani wao Yanga pia kushidwa kufunga mabao mengi, raundi hii imeleta kikosini mabao zaidi ya 40.

Msimu uliopita licha ya kushindwa kutwaa makombe hayo ilisumbuliwa na uhaba wa mabao ikifunga 41 tu na kuruhusu 14 jambo liliolowaumiza vigogo wa Simba na kuamua kusaka washambuliaji wapya ambao msimu ujao wataongeza mabao hayo na kuwafurahisha mashabiki wake.

Jina la kwanza kwa Simba ilikuwa ni mshambuliaji wa Vipers ya Uganda, Cesar Lobi Manzoki aliyefunga mara 18 kwenye mechi 29 na kuibuka mfungaji bora wa timu na kutwaa tuzo tano ikiwemo ya mchezaji bora wa ligi hiyo.

Manzoki hajajiunga na kambi kutokana na mambo ya kiutawala lakini takwimu zake zinaonyesha dhamira ya Simba msimu ujao. Msimu uliopita aliyeongoza kwa mabao Simba ni Kibu Denis (mabao nane tu). Sambamba na Manzoki, Simba pia imeshusha mashine nyingine za mabao, kiungo mshambuliaji fundi Mghana Augustine Okrah aliyemaliza msimu na mabao 14 kwenye ligi na mabao nane kwenye Kombe la Shirikisho la nchini kwao akiitumikia Be-che-m Utd iliyomaliza ya tatu ligi kuu.

Mzambia Moses Phiri ni mashine nyingine mpya ya mabao ndani ya Simba kwani msimu uliopita akiwa Zanaco alifunga mabao 14 na msimu mmoja nyuma aliibuka mfungaji bora wa ligi ya Zambia akipachika mabao 16. Pia yupo Habib Kyombo aliyefunga sita msim uliopita.

Wakati huo huo, uongozi wa Simba umefafanua kiungo Sadio Kanoute kuchelewa kambini Misri ni kujaa kwa pasipoti yake ya kusafiria.

SOMA NA HII  DAKIKA SITINI ZA PABLO MAZOEZINI SIMBA BALAA...ANOGEWA NA MAVITUZI YA AJIB, MKUDE..CHAMPION LEO...