Home Geita Gold FC KUELEKEA MICHUANO YA CAF NA LIGI MSIMU UJAO…GEITA GOLD WAFANYA KWELI…WAMNYAKUWA WAWA...

KUELEKEA MICHUANO YA CAF NA LIGI MSIMU UJAO…GEITA GOLD WAFANYA KWELI…WAMNYAKUWA WAWA JUMLA JUMLA…


Baada ya kimya kingi hatimaye Klabu ya Geita Gold imetoka mafichoni na kuanza kuweka hadharani vifaa vyake vipya ilivyovisajili kwa ajili ya msimu mpya.

Geita Gold iliyomaliza ya nne kwenye Ligi Kuu msimu uliopita na kufuzu michuano ya kimataifa imeanza utambulisho wake na Mlinzi wa kulia, Aman George Wawa kutoka Dodoma Jiji.

Beki huyo wa kulia ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja anakwenda kuongeza nguvu katika eneo la ulinzi wa kulia akiungana na David Kameta ‘Duchu’ aliyejiunga na timu hiyo msimu uliopita.

Wawa ametambulishwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo na kusindikizwa na ujumbe wa kusifia kipaji chake.

“Geita Gold FC tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba na mlinzi wa kulia George Aman Wawa,”

“George Wawa alikuwa akitumikia klabu ya Dodoma Jiji, moja kati ya mafundi wa mpira wenye akili ya ulinzi na mbinu za kisasa. Karibu Geita, Karibu saana kwa wawakilishi wa kimataifa,” imesema taarifa hiyo.

Awali Mtendaji Mkuu wa Geita Gold, Simon Shija alikaririwa na Mwanaspoti kuwa walichelewa kutambulisha wachezaji wao kutokana na kuweka sawa masuala ya mikataba na sheria ili kuepuka usumbufu na migogoro inayoibuka baina ya wachezaji na timu.

SOMA NA HII  KILICHOPO NYUMA YA PAZIA ISHU YA JEZI ZA VUNJA BEI NA POLISI TANZANI....WAAMUA KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU...