Home Habari za michezo WAKATI WENZAO WAKIWA WASHANZA KAMBI NA MAANDALIZI YA MSIMU UJAO..NAMUNGO FC WAVUTANA...

WAKATI WENZAO WAKIWA WASHANZA KAMBI NA MAANDALIZI YA MSIMU UJAO..NAMUNGO FC WAVUTANA WAO KWA WAO…


Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutaka kuweka kambi nje ya nchi, Uongozi wa Namungo umefunguka kuwa bado hawajafika muafaka wa wapi ambapo wataenda kuweka kambi kwa ajili ya msimu ujao.

Kikosi hicho kilichoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kwa msimu uliopita kilianza kambi tangu Julai 18 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidadu amesema kuwa hadi sasa bado hawajapata muafaka wa sehemu gani wataweka kambi kwa ajili ya msimu ujao.

“Kwanza tulifikiria kuipeleka timu Kigamboni ama la! na baadae tukawaza kuipeleka nje ya nchi huko Zambia, lakini bado tamati ya mjadala huu lakini tukiamua wapi patatufaa basi tutaweka wazi.”

SOMA NA HII  MO DEWJI AIGA ALIKICHOFANYA BARBARA KWA YANGA...NAYE KAIBUKA NA HILI HADHARANI...